Twataka maji,Jira, yaambiwa serikali ya kaunti ya Kilifi

Wakaazi wa Jira kaunti ndogo ya Ganze wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kuwaanzishia mradi wa maji kama maeneo mengine ya kaunti hiyo ili kuwakinga dhidi ya maradhi yanayotokana na maji machafu.

Wakiongozwa na Kadzo Charo wanawake katika eneo hilo ambao ndio waathiriwa zaidi wa ukosefu wa bidhaa hiyo wamesema kuwa hali hiyo imewasababishia maradhi kwani hunywa maji machafu kutoka kwa kisima kimoja kinachoelekea kukauka katika eneo hilo.

Naye waziri wa maji katika serikali ya kaunti ya Kilifi Kiringi Mwachitu amesema kuwa mikakati inaendelezwa ili kutatua tatizo hilo kwa manufaa ya wakaazi wa eneo hilo kama ilivyo kwenye maeneo mengine hivi punde ikiwa eneo la Mrima wa Ndege.

Mwisho

Total Views: 335 ,