Tuwape vijana ajira, wasema wasomi katika chuo kikuu cha Pwani

Wachanganuzi wa maswala ya kijamii na maendeleo katika chuo kikuu cha Pwani kaunti ya Kilifi wametaja ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana hapa pwani kuwa sababu kuu dhidi ya kuchipuka kwa magenge ya uhalifu katika eneo hili.

Katika mahojiano ya pekee na Pwani Fm,Prof Halim Shauri mmoja wa wachanganuzi hao amesema kuwa kuna haja kwa serikali za kaunti hapa Pwani kuhakikisha kuwa zinaweka mikakati ya kubuni nafasi za ajira ili kukabiliana na swala hilo.

Mwisho

Total Views: 467 ,