Tutakabiliana na njaa vilivyo asema rais Uhuru

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa serikali itatumia shilingi bilioni sita kupunguza bei ya mahindi kwa lengo la kuhakikisha kuwa mlo huo unaopendwa zaidi na wananchi unapatikana bila matatizo.

Rais amesema pesa hizo zitatumika kununua mahindi yote yanayouzwa na wakulima katika msimu huu chini ya mpango wa serikali wa kuhifadhi chakula kwa lengo la kupiga jeki usalama wa chakula na kuhakikisha kuweko kwa bei mwafaka kwa unga wa mahindi.

Akizungumza alipofungua rasmi maonyesho ya kimataifa ya kilimo jijini Nairobi,rais Uhuru aidha amehakikisha kuwa uongozi wake hautachoka kuwaonya wanunuzi dhidi ya kupanda kwa bei ya vyakula.

Amedokeza kuwa katika mwaka huu wa kifedha serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa wizara ya kilimo ,mifugo na uvuvi ili kufadhili mipango itakayopiga jeki kilimo kwa manufaa ya usalama wa chakula nchini.

Mwisho

Total Views: 220 ,