Tusker yasalia Kileleni mwa Ligi

Ligi kuu ya humu nchini iliingia mechi zake za 19 wikendi hii huku timu kadhaa zikijizatiti kuandikisha ushindi ili kujinasua kutoka orodha ya matokeo mabaya wakati huu wa awamu ya pili ya ligi kuu ya kitaifa.

Katika vilabu vilivyo katika uongozi wa tau bora katika jedwali Klabu ya Gor pekee ndio iliandikisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Nairobi city stars huku viongozi wa ligi hiyo wanamvinyo Tusker fc wakipata sare kapa na Sofa paka huku Mathare United wakititikwa mabao 2-0 na Thika united.

Aidha wawakilishi wa Pwani Bandari walipata ushindi wao wa kwanza katika awamu ya pili ya ligi ya kitaifa baada ya kuizima Muhoroni mabao 2-0.

Kwa sasa klabu ya tusker inaongoza ligi kwa alama 37, gor inashkilia nafasi ya pili kwa alama 34 huku Mathare wakishika nafasi ya 3 kwa alama 31 huku wawakilishi wa pwani Bandari fc wakishika nafasi ya 11 kwa alama 23.

Total Views: 295 ,