Jopo la Tunoi lakamilisha vikao vyake

Jopo linalomchunguza aliyekuwa jaji wa mahakama ya juu Philip Tunoi limekamilisha vikao vyake.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Sharad Rao, alisema hawana mamlaka kisheria kuendelea na uchunguzi huo kwani jaji huyo amestaafu. Rao alisema swala la kuhusu iwapo jaji huyo alistaafu kihalali au la, halihusu jopo hilo.

Alisema jopo hilo hata hivyo litawasilisha ushahidi lililokusanya dhidi ya jaji huyo kwa rais Uhuru Kenyatta.

Mwisho

Total Views: 294 ,