Tunawashughulikia waathiriwa wa mafuriko asema Gavana Kingi

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amesema kuwa serikali yake inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa waathiriwa wote wa mafuriko katika kaunti hiyo wanapata msaada unaohitajika ikiwemo kuhamishwa kwa maeneo salama na pia chakula.

Akizungumza nje ya afisi yake alipowasili kutoka kwa kongamano kuhusu ugatuzi,Kingi amesema kuwa zaidi ya watu elfu 3 wanahitaji kuhamishwa hadi maeneo ya juu kufuatia mafuriko yanayotokana na mto sabaki kuvunja kingo zake eneo la Malindi na Magarini.

Amesema kuwa huenda idadi ya waathiriwa ikaongezeka kwani kuna baadhi ya vijiji ambavyo vimezingirwa na maji na kusababisha changamoto mwa maafisa wa kukabiliana na majanga katika kaunti hiyo dhidi ya kuwafikia.

Maeneo ya Garashi,Bate,Madunguni,Goshi na Sabaki ndio yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo huku wakaazi wakionywa dhidi ya kusalia katika maeneo yaliyo chini.

Mwisho

Total Views: 252 ,