Tume ya ardhi yazindua mfumo mpya

Tume ya kitaifa ya ardhi imezindua mfumo wa kidigitali wa kunakili kumbu kumbu za ardhi humu nchini kwa kile ilichotaja kusaidia kuziba mianya ya utapeli ambayo imesabisha kuwepo kwa ufisadi wa kupindukia katika sekta ya ardhi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo waziri wa ardhi Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa utasaidia wakenya kupata habari kwa haraka popote walipo kuhusiana na maswala ya ardhi na wakati huo huo kubadilisha taswira ya  utendakazi katika sekta ya ujenzi ambayo imeshuhudia kuporomoka kwa majengo kadhaa kutokana na ujenzi duni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo Mohammed Swazuri ameongeza kuwa mfumo huo utaokoa wakenya kutoka kwa matapeli ambao wamekuwa wakiwaibia  fedha zao.

Mfumo huo unaogharimu kima cha shilingi bilioni 4 utaanza kutumika  rasmi miaka mine ijayo.

Total Views: 339 ,