Tukubali Matokeo yaelezwa KANU na gavana Kachapin

POKOT GAVANA KACHAPINGavana wa Pokot Simon Kachapin aliyechaguliwa kwa tiketi ya chama cha KANU amekikosoa chama chake kufuatia madai ya kuibwa kwa uchaguzi mdogo wa useneta katika kaunti ya Kericho.
Kachapin badala yake amekitaka chama chake kukubali kushindwa akisema kuwa chama cha JAP kiliibuka na ushindi kwenye uchaguzi huru na wa haki na ulioshamiri ushindani mkali ikitiliwa maanani joto la kisiasa lililoshuhudiwa.
Kauli yake inajiri huku chama cha KANU kikisisitiza kuwa uchaguzi huo ambao mgombea wa JAP Aaron Cheruiyot alishinda haukuwa huru na haki na hata kupinga matokeo yake.
Haya yanajiri huku tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikianzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya maafisa wa serikali wanaodaiwa kuhusika kwenye kampeini za uchaguzi huo kinyume cha sheria za uchaguzi.

Mwisho

Total Views: 382 ,