Tuko tayri dhidi ya Ghana- Harambee Sand stars

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Soka ya ufukweni Harambee sand stars Rajabu Babu mapema leo ametaja kikosi cha wachezaji kumi watakaoshiriki mechi dhidi ya Ghana mnamo siku ya jumamosi ufukweni wa bahari ya hindi.

Kwa mujibu wa Kocha huyo kikosi kilikuwa na wachezaji 25 lakini amepumzisha 10 huku 5 wakisalia kama wachezaji wa ziada, na baada ya mechi ya nyumbani na ugenini huko Ghana iwapo wataibuka na ushindi wataelekea nchini Nigeria mwezi disemba kushiriki kwa mechi za kufuzu kwa kombe la Dunia litakalosakatwa katika taifa la Bahamas.

Timu ya taifa ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini hapo kesho ambapo jumatano alhamisi na ijumaa watakuwa ufukweni kufanya mazoezi ya kujiandaa.
Taifa la Usheli sheli ndio mabingwa watetezi ulimwenguni katika soka ya ufukweni..

Total Views: 350 ,