Tuko na ushahidi wa kutosha,wasema mawakili wa muungano wa NASA

Muungano wa NASA kwa mara nyengine umesisitiza kuwa una ushahidi wa kutosha wa kudhibitisha kuwa uchaguzi mkuu wa urais ulikumbwa na kasoro chungu nzima.

Kupitia mawakili wake wakiongozwa na Seneta wa Siaya James Orengo muungano wa NASA Umesema kuwa una mengi ya kushangaza kuhusiana na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Akizungumza na wanahabari nje ya mahakama baada ya kuwasilisha ,wasilisho lao kwa maandishi kufuatia itikio la jana la rais Uhuru na tume ya IEBC,Orengo amesema utata wa uchaguzi katika ushahidi wao unaibua mseto wa hisia kuhusiana na uhalali wa uchaguzi.

Kadhalka mgombea urais kwa tiketi ya muungano wa Thirdway Ekuru Aukot kupitia mawakili wake pia amewasilisha ombi la kutaka kuhusishwa kwenye rufaa hiyo ya NASA akisema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.

Mwisho

Total Views: 263 ,