Tufuate sheria kwa utatuzi wa utata wa ardhi Kilifi,asema Mng’aro

Viongozi katika kaunti ya Kilifi wamewaomba wananchi kutatua mzozo wa ardhi unaoikumba kaunti hiyo kwa njia ya amani na ya kisheria badala ya kutumia mabavu.

Mbunge wa Kilifi kaskazini, Gideon Mng’aro asema kuwa serikali imeanzisha harakati za kutatua mzozo wa ardhi katika kaunti hiyo.

Aidha aliwaomba wananchi walio na stakabadhi za kuonyesha utaratibu wa ardhi zilizo na utata kujitokeza ili kupeana mwafaka katika utatuzi wa sakata ya ardhi katika kaunti hiyo.

Naye mwakilishi wa wadi ya Sokoni Lawrence Kilabo alisisitiza utumizi wa sheria katika utatuzi wa ardhi hiyo.

Wawili hao walikuwa wakizungumza katika hafla ya kupeana madawati 61 na hundi ya kima cha milioni moja itakayogharamia ukarabati wa madarasa katika shule ya msingi ya mnarani.

Mwisho

Total Views: 464 ,