Taylor Swift Na Calvin Harris Maji Na Mafuta

 

Muimbaji wa Marekani Taylor Swift na mpenzi wake Calvin Harris watengana baada ya kukaa kwa mahusia kwa miezi 15.

Mtu wa karibu na wawili hao ameliambia jarida la People kuwa uhusiano huo haungeweza kudumu kwa sababu haukupangiwa kudumu.

Chanzo kilicho karibu na Taylor kimethibitisha kwa DailyMail.com kuwa ripoti hizi za People ni za kweli. E! News imedai kwa Harris ndiye aliyempiga chini Swift.

Tofauti kubwa ya ratiba zao ni sababu za kuachana. “It seemed like they were more friends than lovers,’ kimesema chanzo.

Huyo anakuwa mwanaume wa nane kuachana na Taylor Swift.

Hawa ni wanaume wengine waliowahi kuwa na uhusiano na muimbaji huyo ambapo wote hakudumu nao sana.

Joe Jonas (2008)
Lucas Till (2009)
John Mayer (2009 – 2010)
Taylor Lautner (2010)
Jake Gyllenhaal (2010 – 2011)
Conor Kennedy (2012)
Harry Styles (2012 – 2013)

Total Views: 500 ,