‘Tangaza Msimamo Wako Kuhusu Ruto’ Wazee wa Riftvalley Wamwambia Ruto

Baraza la wazee la RiftValley linamtaka rais Uhuru Kenyatta kutangaza msimamo wake wa iwapo bado anaunga mkono azma ya naibu wake William Ruto ya kuwania urais mwaka 2022 au la.

Kwenye hatua inayoonekana kuwakasirisha wendani wa rais Kenyatta,wazee hao wanamtaka kiongozi wa taifa kutangaza msimamo wake kuhusu azma ya Ruto ambayo imeanza kuleta nyufa na kutishia kusitisha kusambaratisha chama cha Jubilee.

Wazee hao wakiongozwa na Gilbert Kabage walizungumza baada ya mkutano wa saa tatu katika kaunti ya Nakuru ulioitishwa kujadili kuhusu mvutano ndani ya chama hicho miongoni mwa masuala mengine.

Total Views: 145 ,