TAMADUNI MOMBASA

Washikadau na wanaharakati wa kimaendeleo  kaunti ya Mombasa wameitaka serikali ya kaunti na waziri ya utalii nchini kuhakikisha vituo vyote vinavyohusika na maswala ya utamaduni vinaboreshwa kama njia mojawapo ya kuvutia wageni.

Akizungumza na wanahabari mwanaharakati wa maswala ya kimaendeleo kutoka ziwa la ng’ombe Ben Oluoch amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo yanatakiwa kutambuliwa kama vituo vya utamaduni.

Aidha amedokeza kwamba makundi mengi ya waimbaji nyimbo za kitamaduni yameanza kusambaratika na utamaduni kuanza kufifia katika ukanda wa pwani.

Picha hisani.

Total Views: 10 ,