Tahadhari ya Kipindu Pindu nchini

Taasisi ya matibabu nchini KEMRI imetoa wito kwa wakenya kuwa waangalifu zaidi kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulioathiri baadhi ya kaunti nchini ambapo jumla ya watu watatu wamepoteza maisha na wengine kulazwa.

Mtafiti katika taasisi hiyo Daktari John Kiiru amewataka wakenya wanaoishi katika maeneo yaliyoathirika na yale yaliyo na uwezo wa kukumbwa na mkurupuko huo kutumia fursa ya chanjo inayotolewa ambayo hudumu kwa mda wa kati ya miezi sita na mwaka mmoja.

Dkt Kiiru aidha amesema kuwa upungufu wa maji unaoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo nchini umechangia pakubwa mkurupuko huo huku akiwataka wananchi kutibu maji wanayotumia nyumbani.

Mwisho

Total Views: 303 ,