SUPKEM NA KONDOMU

Mwenyekiti wa baraza la ushauri kwa waislam SUPKEM tawi la Changamwe Mustafa Simiyu Bakari amesema kuwa utumizi wa mipira ya kondomu unaoshinikizwa mashuleni ni kinyume na maadili ya kidini.

Akizungumza na wanahabari Sheikh Bakari amesema kuwa kumpa mtoto kondomu ni sawa na kumpa silaha hatari ambayo haifai hivyo akaitaka serikali kurudi nyuma na kusitisha hatua hiyo.

Wakati huo huo mwakilishi wa wadi ya Chaani gatuzi dogo la Changamwe Junior Kyaka Wambua amesema kuwa hatua hiyo itachangia kuongezeka kwa vitendo vya ngono katika shule hivyo kuchangia kudorora kwa viwango vya elimu.

Picha kwa hisani.

 

Total Views: 61 ,