Sserenkuma azima kiu ya mabao

Jumla ya mechi 5 zimesakatwa hii leo ambapo Muhoroni youth wameilaza chemelil bao moja kwa sufuri ,ushuru wakailaza western stima 3-1, KK homeboys wakaridhika na sare ya 1-1 dhidi ya wanajeshi wa ulinzi huku wawakilishi wa Pwani Bandari fc wakitoka sare ya kufungana 1-1 na vijana wa thika United.

Sare ya bandari ndio ya kwanza kwa kaimu kocha Ken Odhiambo ambaye anashikilia usukani baada ya kufurushwa kwa Twahir Muhiddin.

Bao la bandari lilitiwa kimyani na nyota Dan Sserenkuma likiwa ni bao lake la kwanza tangu asajuiliwe na klabu ya Bandari huku Thika united wakipata la kusawazisha kupitia mchezaji Eugene Mukangula.

Kwa sasa bandari wanashikilia nafasi ya 10 wakiwa na alama 18 baada ya kucheza mechi 15.

Total Views: 358 ,