Sitalegeza kamba,asema Nkaissery

Waziri wa maswala ya ndani Joseph Nkaissery amepuzilia mbali madai kuwa anatumia vibaya mamlaka yake akisema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua viongozi wanaotishia usalama wa taifa hili.

Akiongea alipozuru vituo vya polisi vya Kajiado na Kitengela ,Nkaissery ametoa wito kwa viongozi kuwa waangalifu dhidi ya matamshi yao ikizingatiwa kuwa serikali iko macho kuhakikisha kuwa hawawachochei wananchi kwa vyovyote vile.

Amesema kuwa ana uzoefu wa kutosha kwenye maswala ya usalama na kwamba amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria huku akipuuza mbai wa kutekeleza majukumu yake kwa kiimla.

Mwisho

Total Views: 476 ,