Sitafika mbele ya kamati hadi Sonko achukuliwe hatua asema Kidero

Gavana wa kaunti ya Nairobi Dr. Evans Kidero amesema hatafika tena mbele ya kamati ya bunge kuhusu uwekezaji wa umma iwapo seneta Mike Sonko hataadhibiwa kwa madai ya kumtusi wakati wa kikao cha wiki iliyopita.

Kwenye barua kwa spika wa seneti Ekwe Ethuro ,Kidero amesema atafika katika mahakama ya juu kutafuta ushauri wa kupinga kinga inayopewa wabunge iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya  Sonko.

Mwisho

Total Views: 334 ,