SIO POLISI WOTE WATAKAOHAMA KWENYE NYUMBA VITUONI,ASEMA IPARA

Sio polisi wote watakaohama kutoka nyumba za polisi katika vituo vya polisi nchini.

Haya ni kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara.

Ipara anasema kuwa polisi ambao wamelazimika kutafuta makao nje ya vituo vya polisi kulingana na agizo la serikali,ni wale ambao hawakuwa na  nyumba kwenye vituo hivyo.

Aidha Ipara amesema kuwa maafisa walioamua kujiunga na jamii wameridhia mpango huo.

‘’Wale hawana makao katika line ya polisi ndio watakaohama,wale wako na nyumba wataishi kule na watakuja kulipa pesa ambaye imepitishwa na ministry of housing’’

Waakati huo huo afisaa huyo mkuu wa polisi amesistiza kuwa hatua ya maafisa wao kujumuishwa katika  jamii itaboresha pakubwa usalama.

Maafisa hao wataweza kujiunga na kamati za nyumba kumi na kamati nyingine za ukiusalama.

‘’Maafisa wetu wanafurahia kutoka vituo vya polisi kwenda kuisha pamoja na watu wa kawaida,kufikia sasa hatujapata matatizo yoyote wananchi wametuunga na wametukubali’’

Mnamo Septemba mwaka jana rais Uhuru Kenyatta aliagiza kuwa maafisa wa polisi wahame kutoka nyumba wanazoishi vituoni na badala yake watapewa marupurupu ya kulipa kodi.

Total Views: 102 ,