Sio Bajeti Yetu wasema baadhi ya Wananchi

Wakenya wengi wanaamini kuwa bajeti iliyosomwa haina uzito wowote katika maisha yao ya kila siku kutokana na uwezekano kwamba huenda garama za maisha zikapanda zaidi.

Kulingana na maoni tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi asilimia kubwa ya wakenya tuliowahoji wanasema kuwa bajeti hiyo haina umuhimu kuwa wakidai kuwa pesa nyingi katika bajeti hiyo zimetengewa mishahara ya wafanyikazi wa serikali na sio miradi.

Mtaalam wa maswala ya uchumi Ramogi Odhiambo anasema kuna hofu kuwa huenda bajeti hiyo ikasababisha kupanda zaidi kwa garama za maisha kutokana na mikakati ya serikali ya kutafuta pesa za kugaramia bajeti hiyo nono ikiwemo kupandisha ushuru wa bidhaa.

Wamesema kuwa ili serikali kuweza kufikia kiwango cha makadirio hayo italazimika kuongeza bei ya bidhaa za mwananchi kupitia ushuru jambo linalosababisha ugumu wa maisha kwa wakenya.

Waziri wa fedha Henry Rotich alisoma makadirio hayo ya bajeti ya shilingi trillioni 2.3 yanayolenga kufadhili maendeleo na garama za kuendesha shughuli za serikali.

Mwisho

Total Views: 382 ,