Sijapinga ujenzi wa kambi ya Jeshi asema,Timamy.

TIMAMYGAVANA wa Lamu, Issa Timamy, amepinga vikali madai kwamba anapinga kuweko kwa kambi ya Jeshi (KDF) katika eneo la Pandanguo, Kaunti ya Lamu.

Kwenye kikao na wanahabari Kisiwani Lamu, Timamy, alikiri kwamba wanaoeneza uvumi huo ni baadhi ya wanasiasa wanaompiga vita kwa lengo la kujipigia debe kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2017.

Mapema juma hili,Seneta wa Lamu, Abu Chiaba, Mbunge wa Lamu Magharibi, Julius Ndegwa na Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Lamu, Bi Shakila Abdalla, walimkashifu Gavana Timamy kwa kutolichukulia kwa uzito suala la usalama wa Lamu na nchini kwa jumla.

Mwisho

Total Views: 360 ,