Sibanduki ng’o, asema Sossion

Katibu mkuu wa chama cha walimu KNUT aliyesimamishwa Wilson Sossion amesisitiza kuwa bado anasalia kuwa msemaji wa chama hicho akisema kuwa baraza kuu halikufuata taratibu hitajika katika kumuondoa ofisini.

Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya chama hicho ,Sossion amesema kuwa ili kwa afisa aliyechaguliwa kuondolewa ni sharti baraza hilo lipokee ilani kwa maandishi inayoelezea kinaga ubaga agenda husika.

Amesisitiza kuwa ataendelea kutekeleza majukumu yake katika chama hicho bila hofu na upendeleo kauli inayojiri huku mahakama ya leba ikitoa agizo kwa msajili wa vyama vya wafanyikazi dhidi ya kuliondoa jina lake kama katibu mkuu wa Knut.

Jaji Maureen Onyango aidha amekiagiza chama hicho dhidi ya kuchukua hatua zozote za kujaza nafasi ya Sossion hadi ombi lake litakaposikizwa na kuamuliwa tarehe kumi mei.

Mwisho

Total Views: 238 ,