Shirika la Slum Festival latua Mombasa

Shirika moja la kutegeza filamu nchini Slum Film festival kwa ushirikiano na Pwani youth Network , limetoa wito kwa vijana hapa mombasa kujitokeza na kutumia filamu kama fursa ya kueleza hisia zao katika nyanja mbali mbali za maisha.

Slum Film Festival ambayo ina makao yake jijini Nairobi hujihusisha na mada mbali mbali zinazolenga jamii na mazingira wanayoishi hasa mitaa ya mabanda, na hutumia filamu kueleza ulimwengu maswala kadha yanayokumba jamii na kutoa changamoto kuyakabili.

Shirleen Amisi ambaye ni mwelekezi katika shirika hilo anasema wamekita kambi kaunti ya Mombasa wikendi hii kutoa fursa kwa vijana, ambapo wanaonyesha filamu eneo la Bangladesh katika eneo bunge la changamwe , na kauli mbiu ya mwaka huu ni Mazingira mapya.

Aidha wanaangazia swala la mihadarati, gonjwa la ukimwi,mapenzi katika umri mdogo pamoja na ukosefu wa ajira ikiwemo maswala kadhaa yanayokumba jamii kila siku maishani.

Watengezaji filamu hutoa maelezo kuhusu filamu zao ambazo hupigwa msasa na kisha kuzawadiwa katika vitengo mbali mbali vya filamu.

Total Views: 180 ,