shirika la kijamii DZARINO CBO latoa changamoto kwa serikali za kaunti

Shirika moja la kijamii Dzarino CBO limetoa wito kwa wazazi kaunti za Mombasa,Kwale na kilifi kujenga uhusiano mzuri na wanao ili kurahisisha mazungumzo kati yao na kubaini kwa urahisi matatizo wanayokumbana nayo.

Akizungumza katika kikao na wanahabari hapa Mombasa , mkurugenzi wa shirika hilo Elvina Mutua amesema ukali wa wazazi humfanya mtoto kuwa mwoga na vigumu kuweka bayana matatizo anayokuymbana nayo wakati anapokua, hatua ambayo imefanya kuwa v igumu kwa wazazi kutoa nasha kwani hawana ufahamu kamili kuhusu hali ya watoto wao

Shirika hilo ambalo linalenga akina mama na vijana hasa wasichna limetoa wito kwa serikali za kaunti eneo la pwani kuwajibikia maswala ya akina mama na vijana ili kutoa fursa kwao kujiendeleza maishani na kuwa kielelzo kwa jamii.

Shirika la Dzarino CBO limejikita kuangazia maswala ya familia za mashinani , ikiwemo mayatima ili kuwapa fursa kujikimu kimaisha na kuendeleza familia zao.

Total Views: 187 ,