Shambulizi:Polisi wauawa, Mandera

Jumla ya maafisa watano wa polisi waliuawa huku wengine wanne wakiuguza majeraha hospitalini baada ya gari lao kurushiwa gruneti na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Alshabaab katika eneo la mandera.

Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa polisi katika eneo hilo Job Boronjo amesema kuwa gari hilo la polisi lililosalia majivu lilikuwa likishindikiza basi lililokuwa likielekea Nairobi kabla ya shambulizi hilo katika eneo la Dimu.

Mwisho

Total Views: 448 ,