SGR Tayari kutumika

Matayarisho ya uzinduzi rasmi wa awamu ya kwanza ya reli ya kisasa kati ya Mombasa na Nairobi yamekamilika.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli la Kenya Atanus Maina amesema serikali sasa inajiandaa kuanza kujenga awamu ya 2B ya reli hiyo kati ya Naivasha na Kisumu baada ya Kenya kupata mkopo wa shillingi billion 360 za kugharamia mradi huo.

Mkopo huo ulipatikana wakati wa ziara ya wiki iliyopita ya rais Uhuru Kenyatta nchini China.

Awamu ya pili ya reli hiyo kutoka Nairobi hadi Malaba imegawanywa katika awamu tatu ndogo ambazo ni awamu ya 2A, 2B na 2C.

Mwisho

Total Views: 274 ,