Serikali yatangaza jumanne tarehe 28 Nov kuwa likizo

Kaimu waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiang’i ametangaza jumanne tarehe 28 Nov kuwa siku kuu ya kitaifa ili kuwapa fursa wananchi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule Uhuru Kenyatta.

Haya yanajiri huku ikibainika kuwa hafla ya kupeana mamlaka haitafanyika kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati andalizi wa sherehe hizo Joseph Kinyua ikizingatiwa kuwa rais mteule ndiye rais wa sasa.

Msajili mkuu wa idara ya mahakama Anne Amadi anatarajiwa kuongoza shughuli ya kiapo kwa rais mteule kabla ya kufuata kwa naibu wake William Ruto.

Mwisho

Total Views: 206 ,