Serikali yapinga madai ya upendeleo dhidi ya wafanyikazi wa SGR

Serikali imetetea usimamizi wa Wachina kwenye shughuli za treni ya kisasa dhidi ya madai kwamba wanawadhulumu wenzao Wakenya.

Hatibu wa serikali Eric Kiraithe anasema Wakenya wana maadili duni ya kikazi na hawapaswi kupaka dosari mradi wa reli ya kisasa hali ambayo huenda ikaathiri utekelezaji mradi huo.

Haya yanajiri siku kadhaa baada ya ufichuzi kwamba wataalam wa hapa nchini wanabaguliwa na kupewa kazi za vibarua kwenye treni hiyo miongoni mwa madai mengine.

Kiraithe anasema wafanyikazi wa mradi wa reli ya kisasa hawaruhusiwi kutoa malalamishi yao kupitia mitandao ya kijamii na badala yake wapasa kutafuta usaidizi kutoka kwa ofisi za serikali zilizoidhinishwa endapo wanahisi kudhulumiwa.

Alisema kila dai la utovu wa maadili miongoni mwa Wachina litachunguzwa.

Mwisho

Total Views: 113 ,