Serikali yapiga marufuku Maandamano nchini

Serikali imepiga marufuku maandamano ya umma jijini Nairobi,hapa Mombasa na Kisumu notisi inayoanza kutekelezwa mara moja.

Akiwahutubia wanahabari katika jumba la Harambee,kaimu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i amesema kuwa hivi karibuni wizara yake itachapisha masharti yatakayopena muongozo wa maandamano ya umma ili kuepuka kutatizwa kwa haki za wengine.

Amesema serikali haiwezi ikahitilafiana na maandamano ya amani ila haitaruhusu uharibifu na wizi wa mali ya watu wengine kama iilivyoshuhudiwa katika siku za hivi karibuni kwenye maandamano ya NASA.

Kadhalka amesema kuwa afisa mkuu mtendaji wa NASA Norman Magaya atawajibikia wizi na uharibifu wa biashara ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya NASA hivi karibuni katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Mwisho

Total Views: 151 ,