Serikali yaagiza kufungwa kwa shule ya St Theresa kaunti ya Nakuru kufuatia madai ya udanganyifu katika KCSE

Shule  ya upili ya wasichana ya St. Theresa Senior huko Gilgil, kaunti ya Nakuru usajili wake umefutiliwa mbali na wizara ya elimu kwa madai ya kujihusisha kwenye mienendo isiofaa kwenye mitihani.

Kwenye barua iliyoandikiwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, katibu wa elimu ya msingi Dkt. Belio Kipsang alisema shule hiyo ilihusika katika mienendo isiofaa kwenye mitihani wiki iliyopita kati ya tarehe 9 na 10 mwezi huu.

Shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 109, ilikuwa imewasajili watahiniwa 37 kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.

Dkt. Kipsang alisema uamuzi wa wizara wa kufutilia mbali usajili wa shule hiyo kuanzia tarehe mosi mwezi Disemba mwaka huu umeratibiwa kwenye sheria ya elimu ya msingi ya mwaka 2013.

Mwisho

Total Views: 244 ,