Serikali kuwachukulia wanafunzi wanaozua vurugu shuleni kuwa wahalifu

Katibu wa elimu Belio Kipsang amewaonya wanafunzi dhidi ya kusababisha vurugu shuleni,akisema kuwa watakaopatikana na hatia watachukuliwa kama wahalifu na kukabiliwa vilivyo na mkono wa sheria.

Akizungumza jijini Nairobi Kipsang amesema kuwa uchunguzi dhidi ya taasisi zilizofungwa kufuatia vurugu zilizosababishwa na wanafunzi umeanzishwa na watakaopatikana na hatia watafunguliwa mashtaka ya uhalifu.

Kauli yake inajiri huku akisema kuwa wizara ya elimu inashirikiana na washikadau wengine kuhakikisha kuwa ripoti ya jopo la uchunguzi chini ya uenyekiti wake Clare Omolo kuhusu chanzo cha mizozo hiyo shuleni inatekelezwa.

Haya yanajiri huku shule ya Dagoreti kaunti ya Nairobi na Maranda kaunti ya Siaya zikifungwa kwa mda usiojulikana siku chache baada ya shule nyengine mbili kufungwa ikiwemo ile ya wasichana ya Kisumu na Chabli ya wavulana.

Mwisho

Total Views: 161 ,