Seneta wa Lamu,apoteza kiti chake

Seneta wa kaunti ya Lamu Anwar Loitiptip wa chama cha Jubilee amepoteza kiti chake kufuatia rufaa ya kupinga uamuzi wa mahakama ya juu iliyodumisha ushindi wake mnamo tarehe tisa February mwaka huu.

Wakitoa uamuzi huo jopo la majaji Alnashir Visram,Wanjiru Karanja na Martha Koome wamesema kuwa mlalamishi Hassan Albeity aliibua maswala yaliyofaa kuzingatiwa na mahakama ya juu kuhusiana na kuhesabiwa upya kwa kura na uchunguzi.

Miongoni mwa hitilafu hizo ni kuweko kwa idadi ya wapiga kura walioshiriki ambayo imezidi ile ya waliosajiliwa katika kituo fulani huku majaji hao wakiamua kuwa hitilafu hizo ziliathiri matokeo ya uchaguzi huo licha ya kuweko kwa utofauti w akura 58.

Kwa sasa mahakama hiyo ya rufaa hapa Mombasa imeiagiza tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuandaa uchaguzi mdogo huku mlalamishi aliyegombea wadhfa huo kwa tiketi ya chama cha Wiper akisema amefurahishwa na uamuzi huo.

Mwisho

Total Views: 131 ,