SAFARI YA MWISHO KWA WACHUNGAJI BANDIA NA WAGANGA KILIFI

Kamishna wa kaunti ya Kilifi Magu Mutindika ameagiza kukamatwa na kushtakiwa kwa wachungaji bandia na waganga wanaohusishwa na mauaji ya wazee wanaotuhumiwa kuwa wachawi katika kaunti hiyo.

Mutindika amesema kuwa wachungaji na waganga hao bandia wamekuwa wakiwachochea wananchi kuchukua sheria mikononi mwao ambapo watu 29 waliteketezwa katika kaunti ndogo ya Rabai kwenye kipindi cha miaka miwili kutokana tuhuma za uchawi.

Alizungumza katika warsha iliyoandaliwa na shirika la Haki Yetu ambapo Mkurugenzi wa miradi katika shirika hilo lisilokuwa la serikali Justus Wanyama ametaja maeneo ya Ganda,Matuga,uwanja wa ndege na Matolani kuwa miongoni mwa maeneo athirika.

Total Views: 78 ,