Ruto na jamii ya Kimataifa kuhusu wakimbizi

Naibu wa rais William Ruto alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono uamuzi wa kenya wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyo makao ya wakimbizi wengi zaidi ulimwenguni.

Akihutubia kongamano la ulimwengu kuhusu maslahi ya binadam nchini Turkey, pia alitoa wito kwa jamii hiyo kuisadia kenya na pesa zaidi kwa lengo la kufanikisha mpango huo wa kuwarejesha wakimbizi makwao wengi wakiwa wakutoka nchini Somalia.

Ruto aliweka bayana kuwa kenya iliamua kuchukua msimamo huo ili kukabiliana na ongezeko la mashambulizi ya kigaidi nchini ambayo mengi hupangwa katika kambi hiyo hivyo kuweko kwa haja ya kufungwa kwa maunfaa ya taifa hili.

Ruto aliandamana na waziri wa usalama Joseph Nkaissery na katibu katika wizara ya maswala ya kigeni Monica Juma ambapo pia aliwasilisha ujumbe sawia kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki-Moon na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Mwisho

Total Views: 327 ,