Ripoti ya uhifadhi wa misitu sharti itekelezwe asema Naibu wa rais

Naibu wa rais William Ruto anataka kutekelezwa kwa mapendekezo yaliyotolewa na jopokazi lililobuniwa kuchunguza usimamizi wa rasilimali za misitu nchini na ukataji ovyo wa miti.

Akipokea ripoti hiyo mapema leo Ruto amesema kuwa ripoti hiyo itapeana muelekeo kwa serikali iwapo inastahili kupiga marufuku kwa mda au kikamilifu ukataji wa miti kwenye harakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Jopokazi hilo la wanachama kumi na watano lilibuniwa baada ya serikali kusimamisha ukataji miti kwa mda wa miezi mitatu kufuati uharibifu wa misitu ambao umekuwa ukishuhudiwa katika misitu ya humu nchini.

Kauli yake inajiri huku ikibainika kuwa uharibifu wa misitu nchini ni moja ya sababu kuu zinazochangia upungufu wa mvua na kusababisha kiangazi ambacho kimekuwa kikishuhudiwa mara kwa mara katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Mwisho

Total Views: 223 ,