Rais Uhuru tayari kutia sahihi mswada wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi

Rais Uhuru Kenyatta leo amepokea mswada wa marekebisho ya sheria za uchaguzi wa mwaka wa 2017 uliopitishwa na mabunge yote mawili na ana siku kumi na nne kutia sahihi na kuwa sheria.

Viongozi wa wengi katika bunge la taifa na lile la Seneti Aden Duale na Kipchumba Murkomen wamesema kuwa ni wka manufaa ya wananchi kwa rais kudurusu mswada huo na kisha kutia sahihi ili kuwa sheria.

Mapema juma hili rais Uhuru na naibu wake William Ruto walisisitiza kuunga mkono mabadiliko hayo wakisema kuwa ni vyema kuzibwa kwa kila mwanya uliotambulika na mahakama ya upeo kwa usawa wa mazingira ya kiuchaguzi.

Hata hivyo muungano wa NASA unapinga mabadiliko hayo ukidai kuwa ni njama ya serikali ya Jubilee kutekeleza udanganyifu huku mabalozi wa nchi za kigeni wakihoji nia ya mabadiliko hayo majuma kadha kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais.

Total Views: 164 ,