Rais Uhuru Kenyatta kupokea mswada wa kudhibiti sekta ya benki

 

Rais Uhuru Kenyatta leo anatarajiwa kupokea mswada wa marekebisho ya sheria ya mwaka 2015 kuhusu udhibiti wa riba katika sekta ya benki.

Iwapo mswada huo utatiwa saini na kuwa sheria  utawapa wakenya fursa ya kupata mikopo rahisi kutoka kwa taasisi za kifedha nchini.

Baada ya kupokea mswada huo rais atakuwa na mda wa siku kumi na nne kuamua iwapo autie sahihi ama aukatae kwa kuurejesha bungeni.

Total Views: 345 ,