Rais Uhuru Kenyatta awataka wanafunzi kutatua matatizo yao kistaarabu badala ya kuchoma shule

Rais Uhuru Kenyatta amevunja kimya chake na kuwaonya wanafunzi dhidi ya kujihusisha na visa vya uharibifu shuleni ikiwemo uchomaji wa shule jambo linalosababisha mamilioni ya hasara kwa sekta ya elimu.

Rais Uhuru amesema kuwa uharibifu haujakuwa na wala hautakuwa suluhu kwa matatizo yanayoikumba jamii huku akiwataka wanafunzi kumakinika na kuwasilisha vilio vyao kwa njia sawa na inayostahili badala ya kuchoma shule.

Takriban shule 70 za upili kutoka maeneo mbali mbali ya nchi zimeshuhudia visa vya kuteketezwa na kusababisha wanafunzi kusalia nyumbani huku washikadau katika sekta ya elimu wakigonga vichwa katika kutafuta suluhu dhidi ya tatizo hilo.

mWISHO

Total Views: 482 ,