rais Uhuru Kenyatta awataka wabunge kupitisha sheria ya uwakilishi wa jinsia

Rais Uhuru Kenyatta amemtaka kiongozi wa walio wengi katika bunge la Taifa Aden duale kushinikiza kupitishwa kwa mswada wa kuwepo na uwakilishi wa thuluthi mbili ya jinsia katika bunge la Kitaifa wakakti ambapo litarejelea vikao vyake mnamo tarehe 9 mwezi Mei.

Akizungumza mjini Kisumu msemaji wa serikali Manoah Esipisu, amesema rais Kenyatta ana imani kuwa bado bunge la taifa liko na nafasi ya kupitisha mswada huo kuwa sheria kabla ya kipindi chake kukamilika na bunge hilo kuvunjwa.

Wakati huo huo kiongozi wa walio wengi katika bunge la taifa Aden Duale,amemhakikishia rais kuwa mswada huo utapitishwa huku akiwataka wabunge wenza  kuunga mkono ili kuhakikisha ongezeko la viti maalum katika bunge hilo.

Total Views: 269 ,