Rais Uhuru awataka Wakenya kuiga mfano wa Matiba

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri na wakenya wengine waliohudhuria ibaada ya wafu ya Kenneth Matiba katika kanisa la All Saints Cathedral jijini Nairobi.

Akizungumza wakati wa ibaada hiyo,rais Uhuru amesema kuwa wakenya watamkosa sana mwendazake Matiba ila hawatasahau kutokana na ukakamavu wake na juhudi zake za kushinikiza demokrasia katika ulingo wa kisiasa nchini hasa miaka ya tisaini.

Rais ameongeza kuwa kuna funzo katika maisha ya Matiba kwa wakenya wote hasa viongozi ambao wanastahili kujiuliza kile wanachohitaji kukumbukwa nacho huku akitoa wito kwao kuwafunza vijana watakaochukua uongozi kama Matiba alivyofanya.

Kwa upande wake naibu wa rais William Ruto aliyehudhuria ibaada hiyo pia amemtaja Matiba kuwa shujaa ambaye kujitolea kwake kwa ajili ya demokrasia nchini imekinufaisha kizazi cha sasa cha wakenya.

Mwisho

Total Views: 208 ,