Rais Uhuru awataka CORD Kuheshimu Sheria

Rais Uhuru Kenyatta ameutaka upinzani kufuata sheria ikiwa kwa hakika unataka marekebisho ya tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC.

Rais Uhuru alisema kwamba hana mamlaka ya kuvunja tume ya IEBC akiongeza kusema kuwa sheria iko wazi kuhusu kuvunjwa kwa tume hiyo.

Rais aliukumbusha upinzani kwamba katiba ambayo walishiriki kupitisha,inaweka wazi utaratibu wa kufuatwa endapo mtu anataka kuvunjwa kwa tume ya IEBC huku akisema maandamano na uvunjaji sheria hautasaidia kwa njia yoyote.

Rais Uhuru alikuwa akihutubu katika miji ya Elwak,Wargadud na Rhamu katika kaunti ya Mandera baada ya kuzindua miradi ya maendeleo mwanzoni mwa ziara yake ya siku tatu katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi.

Alisema kwamba nchi hii haitasonga mbele na kuafikia matumaini yake ya kimaendeleo endapo sheria haitaheshimiwa akiongoza kwamba sheria sharti ifuatwe na wote.

Mwisho

Total Views: 329 ,