Rais Uhuru autaka Upinzani NASA kusitisha vitisho dhidi ya IEBC

Rais Uhuru Kenyatta ametaja vitisho vya upinzani dhidi ya tume huru ya uchaguzi na mipaka na idara ya mahakama kuwa dhihirisho la uoga na uongozi wa ki-imla.

Rais Kenyatta alisema Kenya inaongozwa na demokrasia inayompatia kila Mkenya uhuru wa kufanya maamuzi bila ya kutoa vitisho kwa asasi za serikali.

Rais alitaja tisho la upinzani la kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti ikiwa tume ya IEBC haitatekeleza matakwa yake kuwa pingamizi kwa mfumo wa amani wa uchaguzi.

Rais alikariri kujitolea kwake kudumisha demokrasia na kuimarisha maisha ya Wakenya wote huku akisema hatatishika katika azma yake ya kuunganisha taifa.

Alisema haya wakati wa mkutano wa wajumbe wa chama cha Democratic ambao walimuidhinisha kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Mwisho

Total Views: 278 ,