Rais Uhuru atangaza kuondolewa kwa Ada za mtihani wa kitaifa kwa shule za kibinafsi kama ilivyo kwa shule za umma

Serikali imeondoa ada zinazotozwa watihaniwa kwa usajili wa mitihani ya kitaifa miongoni mwa shule za kibinafsi nchini.

Akitoa tangazo hilo kutoka ikulu ya Nairobi,Rais Uhuru Kenyatta aidha amesema kuwa hakutakuwako na utathmini upya wa muongozo wa karo shuleni mwaka huu ikizingatiwa kuwa serikali imeweka mikakati ya kuweko kwa rasilimali za usimamizi wa shule nchini.

Amesema kuwa pesa zilizotengewa elimu bila malipo kwa shule za upili za kutwa ambazo ni kiwango cha bilioni 29 katika mwaka huu wa kifedha zinatosha kukabiliana na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili nchini.

Mwisho

Total Views: 369 ,