Rais Uhuru Ataka Maafisa wa Usalama na wale wa Ugatuzi Kushirikiana.

Rais Uhuru Kenyatta amewataka maafisa wakuu wa serikali na wale usalama katika ngazi za kaunti kushirikiana vilivyo na serikali za kaunti ili kufanikisha ugatuzi.

Rais amesistiza ushirikiano wa karibu baina ya maafisa hao na serikali za kaunti ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wakenya.

Wakati huo huo kiongozi wa taifa amewataka wakuu wa usalama katika maeneo yao kuhakikisha wametoa usalama kwa raslimali za kitaifa,kama njia moja wapo ya kuboresha uchumi.

Ametoa shinikizo hizo alipokutana na maafisa hao katika ikulu ya Mombasa mapema leo

Total Views: 99 ,