Rais Uhuru ashinikiza ushirika kati ya serikali kuu na zile za kaunti

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa kipau mbele miongoni mwa agenda zake nne ni ukuzaji wa sekta ya uzalishaji nchini kwa lengo la kuongeza mchango wake kwa pato la jumla nchini kutoka asilimia 9 hadi kumi na tano.

Akizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa kongamano kuhusu ugatuzi mjini Kakamega,rais amesema kuwa hili linaweza likaafikiwa iwapo serikali ya kitaifa na zile za kaunti zitashirikiana na kutatua changamoto ibuka kwa manufaa ya taifa hili.

Ametoa wito kwa serikali za kaunti kuainisha ushuru wote unaotolewa na wenye biashara ndogo ndogo kwa lengo la kuunga mkono Agenda ya uzalishaji bidhaa nchini huku akitaka kutumika vyema kwa ushuru unaokusanywa kwa manufaa ya wananchi.

Kadhalka amesema kuwa ni wakati sasa kwa taifa kutumia uvumbuzi hitajika sawia na utumizi wa mashine katika kilimo nchini kwa lengo la kufanikisha kushuka zaidi kwa garama ya chakula nchini.

Mwisho

Total Views: 225 ,