Rais Uhuru Aonya Waandamanaji ,CORD

Rais Uhuru Kenyatta ameonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayeharibu mali ya umma au binafsi kwa madai ya kuendesha maandamano ya amani dhidi ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Rais Uhuru aidha amewataka wote wanaoshiriki maandamano hayo yanayoendeshwa na upinzani kutumia busara yao vilivyo sawia na kukoma kuwachokoza maafisa wa usalama kwa kuwarushia mawe akisema kuwa watajilaumu wenyewe.

Akingumza mjini Machakosa,Amedokeza kuwa upinzani hauko tayari kwa mazungumzo kinyume cha ulivyodai awali akisema kuwa hata baada ya serikali kuteua wabunge kwenye kamati maalum ya bunge upinzani haujaonyesha nia ya utayari wa majadiliano hayo.

Rais Uhuru amewaambia viongozi wa upinzani kutokuwa na mawazo ya kumtaka kukaa na kujadiliana nao kuhusu swala la IEBC huku naibu wake William Ruto akitoa wito kwa wanasiasa kukoma kuweka maslahi yao mbele badala ya wananchi.

Mwisho

Total Views: 453 ,