Rais Uhuru amkaribisha waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Rais Uhuru Kenyatta alimkaribisha waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya Nairobi kwenye hafla ya kufana iliyohusisha ufyatuaji mizinga 21.

Netanyahu ambaye yuko kwa ziara ya siku tatu hapa nchini alianza ziara hiyo kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la rais wa kwanza wa taifa hili hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Baadaye Netanyahu akiandamana na mkewe, Sara walitembelea ikulu ya Nairobi ambako alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la wanahewa.

Baadaye alitia sahihi kitabu cha wageni kabla ya kufanya majadiliano ya moja kwa moja na rais Uhuru Kenyatta.

Mwisho

Total Views: 621 ,