Rais Uhuru aelekea Botswana

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Botswana kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Ziara ya rais Kenyatta inayofuatia mwaliko wa mwenyeji wake Ian Khama, inatarajiwa kuboresha uhusiano wa biashara kati ya Kenya na Botswana.

Ndege aliyoabiri rais Kenyatta na ujumbe wake, iliondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili asubuhi.

Rais Alisindikizwa hadi katika uwanja wa ndege na naibu wake William Ruto na maafisa wengine wakuu serikalini.

Mwisho

Total Views: 340 ,