Rais Kenyatta na Odinga kuzuru pwani juma hili

 

Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wanatarajiwa kuzuru eneo la pwani Juma hili huku juhudi za kutafuta kura zikiendelea kuimarika.

Odinga ataanza ziara yake katika kaunti ya Taita-Taveta leo Jumatano mbele ya rais Kenyatta atakayewasili hapa Mombasa kesho Alhamisi kufungua kongamano la chama cha mawakili nchini LSK.

Baada ya kuzuru Taita-Taveta,Odinga ataelekea kaunti ya Kwale ambako atahutubia kongamano la LSK tarehe 19 mwezi huu wa Agosti.

Aidha kinara huyo mwenza wa CORD anatarajiwa kukutana na viongozi kutoka kaunti za Kilifi na Tana River.

Rais Kenyatta pia anatarajiwa kufungua soko lililofanyiwa ukarabaati la Kongowea hapa Mombasa na pia kukutana na viongozi wa eneo hili la Pwani.

Kabla ya ziara ya Odinga katika kaunti ya Taita-Taveta wawakilishi wa wadi wamekuwa wakilalamikia kutoshauriwa  kuhusu ziara ya kiongozi huyo, baadhi wakitishia kuisusia.

Total Views: 407 ,